Laana
- Serah Michiro
- Oct 17, 2024
- 6 min read
Tumaini alikuwa msichana mrembo mwenye rangi nyeusi ya kuvutia.Wanaume walimwita cheusi dawa kutokana na urembo wake.Lakini Tumaini hakuwa mwenye furaha ,roho yake ilijaa karaha. Marehemu babake mzazi kaaga dunia Tumaini akiwa umri wa miaka mitano tu na sasa amo miaka kumi na nane.Tangu kuaga kwake,tumaini na mamake walipitia mateso mingi kwa mkono yake Amu .Amu akamlazimisha mamake Tumaini kumuoa . Kwa unyonge na kwa shingo upande ,akaingia mnaso nakukubali kuwa bibi wa pilli .Wawili,Tumaini na mamake wakalazimishwa kuhamia kwake amu.Tumaini alimchukia amu kwani hakuwa na utu.S moja amu aliwasiri nyumbani akiwa chakari na kumpiga konde bibiye wa kwanza.Alidai bibiye wa kwanza alikuwa gumegume kwani hakutekeleza mahitaji yake.Siku hiyo akamlazimisha mamake Tumaini kulala naye. Alipokataa bilikuli, kwa hasira amu akamzaba kibao na akaachilia siahi.
"Kazi yako ni ipi?nikisema nalitaka nalitaka ,alaa! hii ni mali yangu".amu alisema kwa hasira.
Tumaini aliposikia siahi alishtuka na akakimbia hadi kwenye chumba cha kulala walimokuwa.Mle akampata amu akijaribu kumbamba mamake.Akamnyemelea na kwa hasira akamgonga kogo kwa pasi iliyokuwa juu ya kijimeza moja pindi ulipoingia kwenye lile chumba.Amu akaanguka kwa kishindo kikubwa huku ameshikilia kichwa kwa uchungu.Ngeu ikatiririka tiriri!! kutoka kwa kichwa chake na kuchafua sakafu.Na hapo ndipo amu akapiga moyo konde.Mamake Tumaini alipoona hayo alibaki mle uso wake ukiwa unejaa kicho ,mshtuko na majonzi.
"mama nisaidie,nimemuua amu,nisaidie tafadhali"Tumaini alisema kwa kicho na majonzi. Bibiye wa kwanza wa amu akaingia na alipoona bwanake kalala chini kama gunia la viazi, huku vazi lake limejaa damu,alianza kupiga siahi akiita majirani.Hapo akajua kuwa Tumaini ndiye aliyemuua mumewe, kwani kwa mkono wa kulia alishika pasi lenye lilikuwa na maruperupe ya damu."Majirani njoo mnisaidie, bwana yangu kauliwa na Tumaini,njooni haraka ."kwa simanzi maria ,bibiye wa kwanza wa mjomba aliwaita majirani huku akipiga siahi.Tumaini aliposikia hayo aliachilia pasi, na mguu niponye akaponyoka na kuenda mafichoni.Majirani wakawandia na kumpata amu maiti,maria mwenye majonzi na mamake tumaini aliyekuwa katika hali ya mchanganyo wa hisia.Maiti yake amu ikachukuliwa na kupelekwa mafuoni.Kisha mamakeTumaini akatiwa mbaroni kwa madai ya kuhusika na kifo cha amu.
Tumaini alikimbia gizani bila kujua alipokuwa akielekea.Alikuwa akipwita kama mbweha na vazi lake lilikuwa limerowa harara. Alikimbia ,akakimbia ,akakimbia.. na kwa jaha nzuri akaliona nyumba la matombe .Paa lake lilikuwa lang'ing'nia na lingeangukaa saa yeyote.Aliingia mle ndani na kuotama kwenye kona moja lenye giza totoro na kutulia tuli ja maji mtungini.Alikuwa na uhakika kuwa wangemtafuta au kumpata kwa nyumba ile .Hata hivyo,aliotama pale kwa uoga kwani ilihofiwa kuwa lile nyumba lilikuwa laishi majini.Kule kjijini majirani walikusanyika na wakaamua kumtafuta Tumaini.Majirani wengine walimwona Tumaini kama habithi ,lakini wengine walijua hakulifanya tendo hilo kwa kusudi.Hilo jambo lilileta zogo.
"Nilijua kuwa msichana huyo hataleta maendeleo huku,ona sasa aliyo yatenda."Jirani mmoja alisema kwa dhalala."Nani wewe kumtoa makosa,yule msichana namjua tangu mchanga ,hakuhirimia kulifanya hilo tendo."jirani wa mbili alisema."Twajua hakulikusudia, lakini alishalifanya lile tendo na kumtoa uhai amu yake.Ama nimekosea wenzagu?"jirani wa tatu alisema.Majirani walishikwa na msisimko na wengi wao wakakubaliana na jirani wa tatu na wa kwanza.Moja kwa moja wakafuatana ja siafu kumtafuta Tumaini.
Tumaini akiwa mle ,alisikia nyayo za watu na akajua alikuwa akitafutwa kwa uchu na chonda.Dhalili Tumaini akashikwa na jakamoyo na kiharara chembamba kikamtoka usoni kwa hofu ya kupatikana.Ghafla bin vu! akahisi mkono mzito kwa mabega yake.Alishikwa na mshtuko karibu aachilie siahi, lakini hilo lingekuwa kosa kubwa.Mkono ule ukamkaba mdomo. Nalo mzingo mbaya ukaupiga pua lake na akaelea. Na hapo ndipo akagundua hakuwa pekee yake.Kinyo mwenye kicha aliwa mle ndani pia.
Wakati huyo majirani walikuwa wamekishachoka kumtafuta na moja kwa moja wakaelekea makwao.Punde tu Kinyo alipo utoa mkono wake Tumaini aliamka kwa ukali "Nini wewe , ebu nikome tafadhali hata hauna adabu ukinishika shika. Wadhani mimi ni parachichi mle sokoni.Hebu tuheshimiane."Tumaini alipomaliza kuongea,Kinyo alimwangalia kisha akaachilia kicheko cha stihizai."Toto umenena kama watu kumi,kumbe toto ndogo kama wewe waweza kuwa na hasira za ndovu mkubwa?"Kinyo alisema kwa utani.
Tumaini alipandwa na hasira na akaelekea kutoka kwenye lile nyumba.
"Ningekuwa wewe toto ,singetoka hapa,nakuahidi ukikanyanga nje tu utakamatwa na waliokuwa wakikutafuta."Kinyo alisema.
Hata kama kinyo alikuwa kichaa alisema ukweli hapo.Ikabidi tumaini arudi alimokuwa na kuvumilia kichaa chake Kinyo.
Punde tu kukaanza kunyesha ,nayo baridi ikaongezeka.Wote wawili walitetemeka tetete!
ja kifaranga aliyenyeshewa. Naye Kinyo akaanza kumtongoza Tumaini.
"Toto unajua wewe ni mrembo,wacha mimi nikuambie. Tangu nizaliwe sijai ona urembo ka wako."Kinyo alinena."Haki Kinyo si una mzaha wewe."Tumaini alisema akicheka.
"Toto ju ya hilo si uniojeshe asali ,leo tu kidogo tu,nakuahidi ukinionjesha ..."Kinyo alisema huku akimsongea Tumaini."Niondokee,una kichaa wewe.Nakuahidi ukijaribu chochote ,nitakuonyesha kilicho mtoa kanga manyoya.Ebo! hebu niondokee."Tumaini alisema kwa hasira huku akitaka kumzaba Kinyo kofi.Kinyo akabaki kwa hali ya mshangao na kichaa chake kikamwonyesha huyu alikuwa moto wa kuotea mbali.Kwa uoga akaondoka polepole na kuenda mbali na Tumaini kisha akalala fofofo!
Tumaini hakushikwa na usingizi usiku huo, alikuwa macho ja pakashume.Kulipo kucha Tumaini alipotea na kwenda mafichoni mapya.Akapita katikati ya msitu na alipokuwa akitembea akapatana na bibi mkongwe aliyekuwa akitaka kuvuka mto.Ule mto haukuwa na daraja na yule bibi akamwomba Tumaini amvukishe mto kwenda ng'ambo lile lingine.
"Tafadhali mwanangu nakuomba unisaidie kuvuka huu mto,naenda kumtembelea mwanangu aliyenizalia kijukuu.Nitashukuruu sana ."bibi akasema kwa upole na unyenyekevu."Sawa bibi nitakusaidia,panda mgongoni na ujishikilie vizuri.Nitang'ang'ana na nakupa neno langu utafika lile ngambo."Tumaini alisema huku amechuchuma ili bibi apande mgongoni.Nyanya akapanda na Tumaini akang'ang'ana kuvuka ule mto .Mwishowe walifaulu kulivuka na wakafika lile ng'ambo lingine."Bibi tumefika unaweza shuka sasa."Tumaini alisema huku akihema kwa uchovu. Lakini nyanya hakushuka mgongoni na akakatalia hapo.Mwanzo Tumaini alifikiria ameaga mgongoni mwake.Lakini la hakuwa, kwani Tumaini alihisi akipumua.
"Bibi kwanini hushuki?tumefika ,waweza enda kwa urahisi sasa kumwona mwanako na kijukuu."Tumaini alisema tena ,huku akitegemea atalishuka mgongo .Lakini wapi,yule bibi alibaki pale pale."Nirudishe uliponitoa na ndipo nitashuka." Bibi alijibu kwa ukali. "Tena hauendi kwa mwanako?Tafadhali bibi nafaa kuondoka haraka iwezakanavyo sina muda wa kupoteza."Tumaini alisema kwa hasira na mshangao."Nakuahidi nitatoka mgongoni ukinivukisha tena lile ng'ambo lingine."bibi alisema akitabasamu.Kwa mara ya pilli walivuka mto,nayo kukawa na mawimbi na maji yakavuma.Tumaini akamuomba yule bibi kushuka mgongoni lakini akapuuza.Wote wawili wakadidimia mle.Tumaini akang'ang'ana kuelea ili kulipata hewa, lakini ghafla bin vu akalihisi mkono ukimrudisha mle tena.Na kicheko kikubwa kikasikika kwote,na hapo akagundua kuwa bibi hakuwa mgongoni .Hapo Tumaini akaishiwa na hewa na mwili wake ukaachwa ukielea mtoni.
Mamake Tumaini alifungwa pingu na kutiwa mbaroni.Mle maisha yalikuwa ya mateso.Alivamiwa na kunguni na seli alilokuwemo lilikuwa ndogo na chafu mithili ya dimbwi la taka.Muda alipokuwa mle alimwombea mwanawe jaha njema."Lipi lakuhuzunisha,unafaa kushukuru sana mwanawe hajapatikana na wewe bado hujaliaga.Jione!, mama mkubwa kama wewe, hata hauna aibu.ebo!"askari mwanamke alisema kwa bezo.Machozi yakamtiritrika chururu! mamake Tumaini.Kwa uchungu akalikumbuka alichokuwa hataki kukumbuka aushini mwake.Hata hivyo akalikumbuka na likamkereketa moyo.
( KISENGELE NYUMA)
Mamake Tumaini alipachikwa mimba na mpenzi wake wa kwanza akiwa umri wa miaka kumi na saba tu.Alipomfichulia siri ,mume yule akali- kana lile mimba.Nyumbani kwao akafurushwa walipogundua .Hakuwa na mbele wala nyuma.Na mwanzoni akalihisi kuavya lile mimba,lakini dhamira yake haikumruhusu kulitekeleza hilo tendo. Alijitia moyo na akatafuta kibarua na akalipata katika shamba la kahawa ambapo kila siku alilipwa shillingi ishirini tu.Akalikumbuka kwa majonzi na uchungu alivyolala nje kwenye vinjia kama chokora na mateso aliyoyapitia.Akakumbuka alipojifungua usiku wa manane bila usaidizi wa mtu yeyote,kwani alikuwa amezoea kujitegemea.Pia akakumbuka alipokusanya pesa zake na kuanza biashara ya kuuza mihogo choma.Hapo ndipo wakapatana na Marehemu bwana yake.
Bwanake alikuwa mwashi na kila walipoenda kupumzika baada ya ujenzi ,angepitia hapo na kununua mihogo yake.Muda uliposonga wakapendana na wakaanza kuishi pamoja kama bwana na bibi.Yule mume akamkubali mamake Tumaini hata baada ya kulijua alikuwa na mtoto mdogo wa miezi mitatu.Wakang'ang'ana na maisha .Siku moja shabuka kubwa likawapata ,Tumaini akiwa mwaka moja akaugua kwa sana.Wazazi wake wakaomba pesa kwa marafiki na familia lakini ng'o hawakusaidika.Tumaini alikaa nyumbani tu akiwa hali mahututi bila kuenda hospitali.Siku moja mamake Tumaini akitoka kwa moja wa marafiki wake kuomba pesa ,aliona jogoo aliyekuwa akizurura tu.Kwa tamaa akainyemelea na kuiiba na bila kuonekana akaenda akaiuza sokoni.Lakini ambacho mamake Tumaini hakujua ,lile jogoo lilikuwa limetiwa alama ndogo nyekundu kwa mguu wake wa kulia.Mle Sokoni bibi mmoja mkongwe akalinunua na kulipeleka nyumbani.
Mwenye Jogoo alipogundua jogoo wake ameibiwa,alianza kuitafuta na waka ahidiana na majirani wengine, atakaye patikana na lile jogoo ata aibishwa mbele ya kijiji kizima.Yule bibi mkongwe alipatikana na lile jogoo na madai yakawa yeye ndiye mwizi.Akaibishwa mbele ya kijiji kizima kwa kuvaa gunia na taili shingoni na kuzunguka kwote akisema hata iba tena.Majirani walimcheka na kumdharau.Alijawa na uchungu moyoni na machozi usoni.Nguvu zilimwisha na akaanguka mbele ya umati ,mamake tumaini alikuwa miongoni wa umati huo."Tafadhali aliyeiba lile jogoo jitokeze mimi nitakusamehe."Alisema huku amelemewa na kwa jitimai kuu.Aligonjea mtu mmoja ajitokeze lakini hakuna aliye.Hili lilimkera moyoni na kabla ya kufa akamwachia laana yule mtu.
"Aliye fanya tendo hili ,maisha yako yatakuwa ya mateso na uchungu."Yule bibi akasema na kisha akaaga.
Majirani walishikwa na butwaa walipogundua kuwa wame adhibu mtu asiye na makosa.Mamake Tumaini alihofia na kutetemeka kwani alijua maisha yake ya baadaye yalikuwa yamelaniwa.Lakini alipuuza kwa wakati huo na haraka alikimbia nyumbani na kuchukua pesa aliyokuwa ameuza jogoo nayo mle sokoni na kumpeleka mwanawe hospitalini akatibiwe.Tumaini akawa sawa na maisha ya kaendelea.Lakini Tumaini alipofika miaka mitano ,babake aliugua ugonjwa wa ajabu.Tumbo lake lilivuvumuka na mwishowe akaaga.Huo ndio ulikuwa mwanzo wa laana ,tena Tumaini kuua amu yake.Ghafla Mamake Tumaini alizinduliwa na askari mnene mfupi."wewe ndiye mamake eeh...haya basi ,mwanawe amepatikana akiwa maiti."alisema kwa bezo Kisha akaanza kupiga gumzo na askari mwenzake.Mamake Tumaini aliposikia hivo alishikwa na kichaa na haraka akavuta bastola kwa mfuko wa nyuma wa suruali ya askari .Mlio wa bastola ndio ulisikika tu.Huo ndo ulikuwa mwisho wa Familia ya tumaini.
Kommentare